Monday , 16th Feb , 2015

Zaidi ya watu 50 wamekamatwa na jeshi la polisi kufuatia vurugu kubwa iliyotokea katika mji wa katoro mkoani Geita.

Chanzo cha vurugu hizo ni mgomo wa wanafunzi wa shule za msingi kilimani, Mkapa na Ludete ambapo walilala katikati ya barabara, kushinikiza kuwekewa matuta kutokana na matukio ya ajali ya mara kwa mara hivyo kutishia usalama wao.

Hata baada ya kuwekewa matuta kuzuia ajali vurugu hizo zilipamba moto kutoka kwa wanafunzi na kuingia watu wazima na kuanza kupiga mawe magari yote yaliyokuwa yakipita barabarani ambapo zaidi ya magari 7 yameharibiwa vibaya na watu kujeruhiwa.

Baada ya muda kuonekana hali imetulia magari yaliruhusiwa kuondoka hata hivyo hali haikuwa shwari ambapo magari yote yalirudi katika kituo cha polisi katoro kwa usalama zaidi.

wilaya ya Geita ameagiza walimu wakuu wote wa shule za msingi zilizohusika na uanzishwaji wa vurugu hizo kushushwa vyeo vyao na hatua mbalimbali za kisheria zizingatiwe.