
Mti wa Mshindwi
Miti hii ambayo imetawala kwenye misitu iliyopo mkoani Kigoma pamoja na maeneo ya nchini Burundi inatajwa na wananchi hawa kuwa na faida nyingi ikiwemo kuhifadhi rutuba ya udongo, kutibu nafaka zisiharibiwe na wadudu, kutengeneza juisi na vinywaji vingine pamoja na mbao zake kutoshambuliwa na wadudu aina yoyote.
Lakini kutokana na umaarufu wa mti huu wakazi hawa wanaeleza kile ambacho ni muhimu kuhakikisha miti hiyo ambayo kwa Tanzania inapatikana mkoani kigoma pekee inahifadhiwa.
Kwa upande wake Afisa Kilimo Kata ya Itaba Halmashauri ya wilaya ya Kibondo Alphaksad Edward, amesema mti huo una manufaa makubwa na kushauri kila mkulima aipande kwenye shamba lake.
Mwaka 2020, 2021na mwaka 2022 Shirika lisilo la kiserikali la Dreamnature Landscaping Organization (DLO) kwa kushirikiana na Wahadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine SUA walilazimika kufanya utafiti juu ya mti huu ambao una sifa za aina yake.