Rais wa Ujerumani Joachim Gauck na Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji mstaafu Agustino Ramadhani
Katika ziara hiyo Rais Gauck amezishauri nchi za jumuiya ya afrika mashariki kuendelea kuimarisha ushirikiano miongoni mwao ikiwa ni pamoja na kukabiliana na changamoto zilizopo bila kukata tamaa na pia kuimarisha misingi ya haki za binadamu.
Wakizungumza baada ya kumaliza mazungumzo ya faragha na Rais huyo, Rais wa mahakama ya Afrika jaji mstaafu Agusitino Ramadhani na katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki dr. Richard Sezibera pamoja na kuishukuru Ujerumani kwa misaada, wamesema ziara hiyo imefungua ukurasa mpya wa ushirikiano na imeongeza chachu ya maendeleo.
Kwa upande wao Naibu Katibu mkuu wa EAC anayeshughulikia miundombinu bi Jeska Erio , spika wa bunge hilo Daniel Kidega, na waziri wa Afrika Mashariki wa Tanzania Dkt Harison Mwakyembe wamesema kuwa Ujerumani ni miongoni mwa nchi chache duniani zinazoonesha kwa vitendo nia ya kuzisaidia nchi maskini zikiwemo za Afrika Mashariki na itakazoendelea kukumbwa na wananchi wote wa nchi wanachama.
Kiongozi huyo amemaliza ziara yake nchini kwa kutembelea hifadhi ya taifa ya serengeti hatua ambayo pia inatarajiwa kusaidia kuhamasisha na kuvutia watalii kutoka ujerumani