Thursday , 3rd Nov , 2022

Rais wa Uturuki amesema kwamba mpango wa kuruhusu usafirishaji wa nafaka kutoka Ukraine utazingatia nchi za Afrika zinazohangaika na usambazaji.

Rais wa Uturuki  Recep Tayyip Erdogan amesema yeye na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy wamejadiliana kupeleka nafaka katika nchi za Afrika.

 Rais huyo amesema kwamba hali nchini Djibouti, Somalia na Sudan si nzuri hata kidogo. Ikiwa kuna tatizo katika nchi nyingine zozote zisizoendelea,usafirishaji utazingatia  nchi hizi

  Makubaliano hayo ya nafaka yalisimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki mwezi Julai, na kumaliza kizuizi cha miezi mitano cha Urusi katika  bandari za Ukraine ambazo zilinasa mamilioni ya tani za nafaka na mafuta ya alizeti na kusababisha bei ya chakula kupanda.

Mkataba huo unamalizika Novemba 19 na wale waliohusika bado wanatakiwa kukubaliana kuongeza muda huo.

Urusi ilikuwa imesitisha uungaji mkono wa mauzo ya nafaka lakini ilikubali wiki hii kuanzisha tena ushiriki wake katika makubaliano hayo.