Wednesday , 2nd Nov , 2022

Wasafirishaji na wafanyabiashara wa nafaka yakiwemo mahindi,mchele namaharage wamesema bei ya nafaka hizo inazidi kupaa juu Licha ya Mamlaka ya usimamizi wa Nishati na maji EWURA kutangaza kushuka Kwa bei kwenye mafuta Kwa mfululizo yani mwenzi wa October na bei mpya ya November.

Utakumbuka siku kadhaa zilizopita nilikuwa hapa katikasoko la nafaka la Tandale Dar es Salaam wafanyabiashara wakibainisha kuwa kupanda Kwa bei kunatokana na vita vya Urusi na Ukraine vilivyosababisha Nishati ya mafuta kupanda na kusababisha nafaka pia kutoshikika.

Mwanahabari wetu ametembelea soko la nafaka Tandale kutazama je Kuna ahueni katika bei za vyakula Mara baada ya Nishati hiyo kuzidi kushuka majibu ya wafanyabiashara sokoni hapo yanaonesha kukata tamaa vyakula zinazidi kupaa juu maharage ya njano yakikosekana sokoni kabisa na mekundu yaliyopo huuzwa Hadi 2500 Kwa kilo mchele ukifika Hadi 3000 huku wafanyabiashara wakisema ukame ndo sasa Tatizo kubwa huko Kwa wakulima..

Baadhi ya wasafilishaji wanasema kushuka Kwa Nishati ya mafuta hakusaidii chochote Kwa sasa Kwa kuwa nafaka zinapanda bei zenyewe kutokana na kuadimika kwake kule mashambani

Huenda sasa kama Taifa tuamue kumgeukia Muumba Ili atupe subira kujua ni njia ipi sahihi ya kuiendea kutokana sasa na kipato kuzidiwa na mahitaji muhimu...