
Mkurugenzi wa huduma za utabiri TMA, Dkt.Hamza Kabelwa
Akitoa utabiri huo kwa niaba ya Mkurugenzi mkuu wa TMA Dkt Agnes Kijazi Mkurugenzi wa huduma za utabiri kutoka TMA Dkt Hamza Kabelwa amesema kutokana na mvua kuwa chache kwenye maeneo mengi ya nchi kuna uwezekano wa kupungua kwa uzalushaji wa mazao ya chakula hivyo wakulima wanashauriwa kupanda mbegu za mazao ya chakula zinazostahamili mvua chache.
Aidha Dkt Kabelwa amezitaka kamati za maafa katika ngazi ya mkoa wilaya na vijiji kuanza kuchukua hatua za haraka kutokana na upungufu wa maji ambao unaweza kupelekea kutokea kwa milipuko ya magonjwa.
Nao baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar es salaam wameulezea utabiri huo kwamba unakwenda kuongeza kasi ya kupanda kwa bei za vyakula kutokana na uhaba wa mvua huku wengine wakieleza umuhimu wa kuanza kuweka akiba ya chakula kuanzia sasa