Monday , 24th Oct , 2022

Ziara ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini Marekani inatajwa kuzaa matunda Mara baada ya hii Leo ujumbe wa wawekezaji 35 kutoka Marekani kufika nchini kuja Tanzania kutazama fursa za uwekezaji Katika maeneo mbalimbali.

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Ziara ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan nchini Marekani inatajwa kuzaa matunda Mara baada ya hii Leo ujumbe wa wawekezaji 35 kutoka Marekani kufika nchini kuja Tanzania kutazama fursa za uwekezaji Katika maeneo mbalimbali.

Ziara hiyo inatajwa kuwa ya kimkakati ikilenga uwekezaji Katika viwanda,utalii na sekta ya Kilimo ambapo sasa wawekezaji hao wamekutana na wadau wa Ndani kutazama Kwa namna gani wao wanaweza kuweka mitaji yao nchini.

Hata hivyo Kwa tafiti za umoja wa mataifa wainataja Tanzania kati ya nchi 10 Afrika ikishika nafasi ya Tisa Kwa kuvutia Uwekezaji.

Kwa muda mrefu wafanyabiashara wengi wa Tanzania wamekuwa wakilalamikia changamoto ya upatikanaji wa mitaji hivyo kupitia ziara hizi sasa zinafungua fursa za uwekezaji Kwa wazawa ambapo wawekezaji hao wamesema wamehamasika na mwenendo na Kasi ya uwekezaji Tanzania.

Hadi sasa ziara hiyo ya kimkakati imelenga kulifanya Africa kuwa kapu la chakula ambalo linaweza kulisha maeneo mbalimbali duniani.