
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Eliamani Sedoyeka
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii Eliamani Sedoyeka alipotembelea mabanda mbalimbali kwenye maonesho ya sita ya kimataifa ya Kiswahili ambapo amebainisha kuwa Utalii unatakiwa kutunzwa ili kuongeza zaidi mapato yatokanayo.
Kwa upande wake Afisa Mhifadhi kutoka Wakala wa Huduma za misitu Tanzania TFS Yusuph Tango ameeleza kuwa kwa sasa wao wanaendelea kufanya utalii wa ikolojia, ambao ni rafiki zaidi kwa mazingira.
Nao wadau wa shughili za Utalii nchini, wamempongeza Samia Sululu Hassan kwa kuifungua nchi hasa kwa shughuli za utalii, wakiahidi kuendelea kujikita zaidi kwenye shughuli utalii kwa manufaa ya taifa letu.
Katika maonesho haya leo, viongozi mbalimbali wamehudhuria, akiwepo Waziri wa Utalii Balozi Dk. Pindi Chana na Naibu Waziri wake Mary Masanja.