Monday , 10th Oct , 2022

Nchi za Tanzania na Kenya zimekubaliana Kwa pamoja kumaliza vikwazo 14 vya kibiashara vilivyosalia kutoka 68 vilivyokuwepo awali Ili kurahisisha biashara Kwa pande zote mbili.

Hatua hiyo imefikiwa Mara baada ziara ya kwanza ya Rais  Kenya William Ruto nchini Tanzania ambaye amethibitisha Kuendeleza msingi uliowekwa na waasisi wake katika nyanja za kibiashara na Sekta mbalimbali.

Rais Ruto amesema vikwazo 54 vilivyoondoshwa vilitoa nafasi ya Kuendeleza biashara ambapo biashara kutoka Kenya Hadi Tanzania ilikuwa Shilingi za Kenya bilioni 31 Hadi 45 bilioni huku biashara ya kutoka Tanzania kwenda Kenya ikikuka kutoka Shilingi bilioni 27 Hadi 45.

"Tumezungumza kama viongozi wenu nia ni kumaliza kabisa vikwazo vya kibiashara vilivyosalia ili watu wetu waweze kufanya biashara na kufurahia ushirikiano huu"amesema Samia suluhu Hassan-Rais wa Tanzania.

Sambamba na hilo imebainishwa kuwa mradi wa kwanza ambao umeridhiwa usafirishaji wa Gesi kutoka Mtwara Dar es Salaam Hadi Mombasa na badae Nairobi mradi unatajwa kupunguza gharama kwenye Nishati.

"Mkataba huu tayari mtangulizi wangu mhe Uhuru Kenyata aliusaini mimi nitaanzia hapo kuhakikisha gesi inafika Mombasa hadi Nairobi niwahakikishie wakenya na watanzania tumekuja kufanyakazi"amesema William Ruto-Rais wa Kenya.

Maeneo mengine yaliyotajwa katika ziara hiyo ni eneo la kukuza uchumi kupitia utaliii, kushirikiana kadhibiti ugaidi ,kukomesha biashara haramu  ya binadamu ambapo wametarajia kufikia December,2022 vikwazo vyote viwe vimemalizika kabla ya Xmas.