
Akizindua ripoti ya utafiti iliyofanywa na watafiti ya mwaka 2022 iliyopewa jina la viwango sawa vya kazi 2022 Joseph Nganga Mkurugenzi wa Ajira kutoka Ofisi ya Waziri mkuu amesema serikali itaendelea kuweka mazingira na kutumia tafiti hizo Ili kuadaa sera na taratibu ambazo zitawasaidia watumiaji wakiwemo walioajiriwa kupitia mitandao.
"ajira ya watu elfu kumi ni wengi mno na kwa taratibu za shirika la wafanyakazi Dunia limeweka vigezo vya mtu kupata kiwango gani Cha malipo hivyo ni Muhimu sasa utafiti huu ukazingatiwa na serikali Ili walioajiriwa kupitia mtandao wakapata malipo yanayowasthili".amesema Joseph
Awali wakiwasilisha changamoto za ubora wa Ajira na huduma mitandaoni utafiti umeonesha kuwa Kuna Tatizo kubwa la mikataba,wafanyakazi hawana bima za ajali, mawasiliano mabaya,kukosekana Kwa uwajibikaji wa Moja Kwa Moja Kwa wanafanya biashara mtandao hivyo sasa kuitaka serikali kuweka sera rafiki, taratibu ambazo zitaweka mazingira mazuri Kwa biashara hiyo kuzidi kuimarika.
Utafiti huo umeonesha zipo kampuni nyingi zikiwa zimeajiri watu wengi ambao endapo serikali haitaweka usimamizi basi watoa huduma wataweza kujipangia chochote