
Mahindi yaliyobadilishwa vinasaba (GMO)
Baraza la mawaziri nchini Kenya limefungua mabilioni kwa kampuni zinazojihusisha na sekta ya viumbe vilivyobadilishwa vinasaba (GMO) baada ya kuidhinisha kilimo na uingizaji wa mazao ya bayoteknolojia katika mabadiliko makubwa ya kisera ambayo yanalenga kuifanya Kenya kuwa na uhakika wa chakula na kuwa na bei ya rafiki.
Rais William Ruto wiki hii aliongoza kikao cha baraza la mawaziri kilichoondoa kusitishwa kwa sera ya 2012 ambayo ilizuia uingizaji wa bidhaa za aina hiyo au kilimo cha wazi cha mazao ya GMO.
Kampuni zinazojihusisha na utengenezaji wa mbegu za GMO zitakuwa miongoni mwa wanufaika wakubwa wa mabadiliko ya sera hiyo ambapo yataweka shinikizo kwa wakulima kupunguza bei au kulazimika kutoka sokoni.