
Bandari ya Ndumbi Ziwa Nyasa
Hayo yamebainishwa na kaimu mkuu wa wilaya ya Nyasa ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbinga Mh. Aziza Mangasongo na kusema lengo la ujenzi wa bandari hiyo ni kwaajili ya kusafirisha shehena ya makaa ya mawe kutoka mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka wilayani Mbinga hadi bandari ya Ndumbi ziwa Nyasa.
“Mradi huu umekamilika kwa asilimia 100,hata hivyo hivi sasa upo katika kipindi cha uangalizi cha mwaka mmoja na mradi upo tayari kwa ajili ya matumizi’’- alisema Mangasongo.
Ameongeza kuwa amesema mradi huo umetekelezwa na Kampuni ya CHICCO ambapo ujenzi wake ulianza Desemba 2019 na kukamilika Februari mwaka 2022.
Aidha, akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Kanali Laban Thomas amesema kukamilika kwa mradi huo kutachochea maendeleo ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma na nchi jirani za Msumbiji na Malawi.