Wednesday , 7th Sep , 2022

Watumiaji wa nishati ya mafuta wameiomba serikali kama upo uwezekano wa kuwaruhusu wafanyabiashara wenye uwezo wa kuagiza  mafuta kuwapa kibali Ili kuleta ushindani katika soko hali itakayopunguza panda shuka ya nishati hiyo.

Kituo cha mafuta

Licha ya kupungua kwa bei ya mafuta iliyotangazwa bado wakazi na watumiaji wa vyombo vya moto wanasema hakuna maajabu kwa kuwa serikali bado imeshindwa kutoa mwongozo ulioonyooka katika masuala ya nishati hii.

Baadhi ya wamiliki wa vituo vya mafuta kwa masharti ya kutorekodiwa wamesema serikali ije na suluhisho kwani wapo wengi wenye uwezo wa kufanya biashara wapewe vibali.

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza sababu ya kushuka bei ni kutokana na kushuka kwa bei katika soko la Dunia ambapo kwa bei elekezi kwa mkoa wa Dar es Salaam kwa mwezi Septemba petroli kwa lita inauzwa shilingi 2969, dizeli 3125 na mafuta ya taa ni 3335 kwa lita.