Mtuhumiwa mmoja wa ujambazi akipakizwa kwenye gari ya polisi
Jeshi la polisi Zanzibar kwa kushirikiana na wafanyabiashara wa machinga walioko darajani Zanzibar wamefankiwa kuwakamata majambazi wawili huku kukiwa na taarifa kuwa mmoja amefariki baada ya kutupiana risasi na kusababisha kizaazaa cha aina yake mjini Zanzibar.
Hali hiyo imetokea baada ya polisi kuanza kuwasaka na kuwafuata majambazi hayo ambayo baada ya kuona wamenaswa wakaamua kukimbia na kuingia maeneo ambayo yanatumiwa na wafanyabishara wadogo wadogo maarufu kwa jina la 'dada njoo'
Baada ya kuingia katika maeneo hayo, ndipo wafanyabishara hao wakaanza kuwanasa nakuwabana majambazi hayo yaliyokuwa katika gari aina ya Noah yenye namba za usajili ambazo inasemekana ni za bandia.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mjini Magharibi Muccadam Khamis amesema polisi bado inawasaka wengine ingawa amesema uchunguzi unaendelea na kuthibitisha kuwepo kwa wananchi wanane ambao walipatwa mshtuko na wako hopitali ya Mnazi Mmoja wakipata huduma za matibabu.
Hata hivyo taarifa zilipatikana mjini Zanzibar zinadai kuwa jambazi moja ambaye anajulikana kwa jina la Khmais Mabunduki na ambaye alikuwa anasakwa na polisi kwa muda mrefu ndiye aliyefariki kutoakna na mapigano hayo, huku bado polisi wakiendelea kuwasaka wengine ambao wako katika mtandao mmoja.