
Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Dkt. Philip Mpango
Makamu wa Rais ameagiza kiswahili kutumika katika mikataba mbalimbali ya miradi ya maendeleo, kwenye maelekezo ya dawa mbalimbali pamoja na mitaa ya barabarani
"Nyaraka za mawaziliano za Wizara na idara zake ziwe kwa lugha ya Kiswahili, mikutano, warsha, mijadala na dhima ziendeshwe kwa Kiswahili"
"Majina ya barabara, mitaa, mabango, fomu za usaili, na maelekezo ya matumizi ya dawa zote, bidhaa na huduma viandikwe kwa Kiswahili"
"Taarifa za miradi na mikataba inayohusu wananchi ni lazima ziwe kwa lugha ya Kiswahili"
Dkt. Mapango ametoa maelekezo hayo leo wakati wa maadhimisho ya siku ya kiswahili duniani ambayo sasa inaadhimishwa Julai 7 ya kila mwaka