Wednesday , 1st Jun , 2022

Mwekezaji wa hoteli za kifahari nchini Marekani, Munir Walji, amewasili nchini kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana, kuhusu uwekezaji wa hoteli za kitalii ambazo zitaongeza thamani katika sekta hiyo.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana akizungumza na Munir Walji Mwekezaji wa hoteli za kifahari Marekani

Katika mazungumzo yake Dkt. Chana,amempongeza mwekezaji huyo kwa uamuzi wa kutaka kuwekeza katika sekta ya utalii hapa nchini na kumuahidi kumpa ushirikiano mkubwa ili aweze kufanikisha adhima yake njema kwa Tanzania.

Hatua hii inakuja ikiwa ni jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, za kutangaza utalii uliopo nchini kupitia filamu ya The Royal Tour  zinaendelea kuzaa matunda nchini.