Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Rais Samia aridhia nyongeza ya mishahara kwa 23.3%

Saturday , 14th May , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia mapendekezo ya nyongeza ya mshahara ikiwemo kima cha chini kwa watumishi wa umma kwa 23.3%. 

Mapendekezo hayo yaliyowasilishwa Ikulu ni mwendelezo wa kikao cha  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alichofanya hivi karibuni mkoani Dodoma na kupokea taarifa ya wataalamu kuhusu nyongeza ya mishahara.

Nyongeza hiyo imefanyika kwa kuzingatia Pato la Taifa (GDP), mapato ya ndani yanayotarajiwa kukusanywa katika mwaka 2022/2023 na hali ya uchumi wa ndani na nje ya nchi.

Kutokana na hatua hiyo katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imepanga kutumia kiasi cha Shilingi trilioni 9.7 kwa ajili ya kugharamia malipo ya mishahara ya watumishi wote katika Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Taasisi na Wakala za Serikali.

Hivyo bajeti ya mishahara ya mwaka 2022/23 ina ongezeko la Shilingi trilioni 1.59 sawa na 19.51% ikilinganishwa na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22. 

Wakati huo huo, Rais Samia amepokea mapendekezo ya kanuni mpya ya Mafao ya Pensheni kama Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) lilivyoomba Mei mosi, 2022.

Mhe. Rais Samia ameridhia na kuielekeza wizara yenye dhamana na masuala ya hifadhi ya jamii kuendelea kushirikiana na TUCTA na Chama cha Waajiri nchini (ATE) ili kukamilisha taratibu za kuhakikisha malipo ya mkupuo ya 25% yaliokataliwa na wadau mwaka 2018 yanapandishwa hadi 33%.
 

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90