Wednesday , 14th Jan , 2015

Msanii wa muziki kutoka kundi la P Unit la nchini Kenya, Frasha ameamua kujiboresha na kupika albam ya peke yake nje ya kundi, hatua ambayo inaziongezea nguvu tetesi zinazoenea juu ya uwezekano wa kusambaratika kwa kundi hilo.

Msanii wa kundi la P Unit la nchini Kenya Frasha

Albam hii mpya ya Frasha itashirikisha wasanii wengine wanaofanya vizuri nchini Kenya, akiwepo rapa Rabbit, Kristoff, STL vilevile Kidum na Eric Wainaina kati ya wengineo.

Tayari taarifa rasmi kutoka kundi hili limekanusha taarifa kuhusiana na kundi hili kutaka kutengana ingawa project hii ya pembeni ya Frasha inatazamwa kama kazi ambayo inaweza kuwaweka mbali wasanii hawa tofauti na ilivyokuwa zamani.