
Kauli hiyo imetolewa na wakazi wa dar es salaam wenye asili ya kabila la Masai ambao ni sehemu ya wahanga wa matatizo mengi ya elimu ambapo wamesema kizazi cha zamani watu wengi waliathiriwa.
"Sisi saizi tumesoma tunashukuru mungu lakini zamani baba zetu walikuwa hawapendi sisi tujue shule" alisema Jeremiah Isaya-Mfugaji pamoja na Yohana Thomas-Mfugaji.
Mara baada ya mtandao wa Elimu Tanzania Tenmet kueleza maandalizi ya wiki hiyo na kugusia uwekezaji wa wa ujenzi wa madarasa mabweni, na nyumba za walimu bado wamesema changamoto ni kubwa hivyo kuwataka wadau mashirika yasiyo ya kiserikali, watunga sera kuja na Mpango kazi kupitia Juma la elimu.
"Tunatamani kuona jamii sasa inakuja kufanya uwekezaji mkubwa Kwa kufanya ujenzi wa mabweni Kwa watu wenye ulemavu Ili wapate unafuu wa kupata elimu"walisema Alistidia Kamugisha-meneja miradi-Mtandao wa Elimu Tanzania pamoja na Dkt Ellen otari-Mjumbe TENMET
Wiki ya elimu itakayoanza tarehe 25-29 mwezi huu wa April wilayani igunga mkoani Tabora inatajwa kuzijadili sera kanuni na sheria ambazo Ili kufikia Mpango wa umoja wa mataifa wa Maendeleo endelevu ambapo kauli mbiu ni tuwekeze katika elimu Kwa elimu bora ukihudhuriwa na mashirika yasiyo ya kiserikali.