Tuesday , 19th Apr , 2022

Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Malapo, amesema kwa mujibu wa ripoti ya CAG imebaini kwamba katika mradi wa kufunga taa za barabarani katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, taa moja ilitakiwa ilipwe kwa shilingi milioni 7.5 badala yake ililipwa kwa shilingi milioni 18.14.

Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Malapo

Kauli hiyo ameitoa bungeni jijini Dodoma, hii leo Aprili 19, 2022, na kuiomba Wizara ya TAMISEMI kufuatilia pesa zinazopelekwa kwenye halmashauri kwa kuwa kuna upigaji mkubwa sana badala ya kuleta tija kwa wananchi.

"Nyinyi kama Wizara mnakazi kubwa sana ya kufuatili hizo pesa, tunaambiwa mawaziri ni vijana maana yake tunatambua mchakamchaka, vijana mnapaswa mkimbie, kama mlikuwa mnakimbia kwa spidi 100 mnapaswa mkimbie kwa spidi 150 hali huko chini sio shwari sana,"amesema Mbunge Tunza