Tuesday , 19th Apr , 2022

Huko Kentucky nchini Marekani, mwanaume anayefahamika kwa jina la Kevin Berling ameshinda kesi yake mahakamani na anatakiwa kulipwa fidia ya Tsh billion 1 baada ya kampuni yake kumuandalia sherehe ya 'birthday' bila kumwambia.

Kevin Berling ana tatizo la 'Anxiety' ambalo humfanya kuwa muoga na mtu mwenye wasiwasi mara kwa mara.

Mwaka 2019 alitoa taarifa kwa bosi wake hataki kushtukizwa na tukio lolote akiwa kazini, na baada ya miezi 10 kampuni yake ilimshtukiza kwa surprise katika siku yake ya kuzaliwa.