Monday , 18th Apr , 2022

Serikali ya imeridhia kuanza kutumika kwa Mfumo wa Kidijitali wa Usahihishaji Mitihani ya Kitaifa ya Ualimu mfumo ulioandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) akifafanua jambo kwa baadhi ya wataalamu waliopo katika majaribio ya usahihishaji mitihani kwa kutumia Mfumo wa Kidijitali ulioandaliwa na Baraza la Mitihani Tanzania.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf amesema mfumo huo utaokoa fedha nyingi zilizokuwa zikitumika wakati wa usahihishaji wa mitihani ya kitaifa.

Waziri huyo amekagua mfumo huo na kueleza kuwa ameridhika na maandalizi yake

“Nimeambiwa Mfumo huu wa usahishaji mitihani ya Ualimu unatarajiwa kuanza rasmi kutumika mwaka huu kwa kusahihisha mitihani ya ualimu ya vyuo vyote na mwakani utaendelea katika hatua nyingiine ya kusahihisha mitihani ya kidato cha sita na tayari waalimu na wakaguzi wameandaliwa na kupatiwa vifaa husika,” amesema Waziri Mkenda.

Mkenda amesema mfumo huo ni wa kwanza katika Afrika na umeandaliwa na vijana wa Kitanzania ambao ni wataalamu kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania ambapo amesisitiza kwamba lengo la Serikali ni kuiona NECTA inafanya shughuli zake zote kidijitali ifikapo 2025.