
Zainab Oladehinde, mwanamke anayetuhumu kutaka kubakwa Zanzibar
Hatua hiyo imekuja baada ya mwanamke huyo kuandika waraka wa tuhuma hizo kupitia mtandao wake wa Twitter, akituhumu kufanyiwa kitendo hicho mnamo mwezi Aprili 2021, alipofika visiwani humo kwa ajili ya mapumziko yake ya kusherehekea sikukuu yake ya kuzaliwa.
Zainab anadai kwamba mwanaume huyo hakufanikiwa kumwingilia kimwili baada ya kumwambia kuwa ni vyema akatumia kondomu kwani yeye ni mwathirika wa VVU na ndipo mwanaume huyo alipoondoka chumbani humo akiahidi kwenda kuchukua kinga hizo.
Zainab ameendelea kudai kwamba, hata alipojaribu kuhitaji msaada wa hoteli hiyo hakupata ushirikiano mzuri jambo ambalo anadai pia hata alipokwenda polisi hakupata msaada stahiki.
Tume ya Utalii Zanzibar, imeeleza kwamba huo sio ukarimu wa Wazanzibari na kitendo hicho si cha kiungwana kwa mtalii yeyote.