Saturday , 16th Apr , 2022

Raia mmoja wa nchini Algeria aliyeshinda bahati nasibu ya dola  270,000 ambazo ni sawa na zaidi ya shilingi milioni 632 za Tanzania, anakwama kuzipata fedha zake akiwa nchini ubelgiji sababu za kukosa vibali halali vya kuishi nchini humo.

Zawadi hiyo ni kubwa sana kulipwa kwa fedha taslimu, na kwamba mtu huyo hana makaratasi ya kuhalalisha yeye kufungua benki nchini humo.  

Rafiki yake wa karibu ambaye alijaribu kuzifuatilia fedha hizo, aliandamwa na kashfa ya wizi wa fedha. 

Mshindi huyo amesema kuwa anazitaka fedha hizo ili ili aweze kuishi nchini Ubelgiji .
"nikizipata hizo fedha nitanunua nyumba ya kuishi huko Brussels. Na pia nitanunua gari,"  amesema mtu huyo ambaye utambulisho wake haujawekwa wazi. 

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 28 hana vitambulisho rasmi kuishi nchini humo, wala hana makazi ya kudumu , kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Ubelgiji.  

 Mwanasheria wa mtu huyo  Alexander Verstraete, amesema kwamba mteja wake  hawezi kufungua akaunti ya benki, huku kampuni ya bahati nasibu imesema kuwa haitafanya malipo hayo nje ya akaunti ya benki.
"Tunatafuta hizo nyaraka ili kuthibitisha uhalali wake wa kuishi huku nchini, , atasiliana na famiilia yake ili kuweka mambo sawa'' amesema mwanasheria huyo  
 
  Mtu huyo aliondoka Algeria miezi minne iliyopita , akisafiri kwa boti akipitia Uhispania , ambapo inasemekana alitembea kwa mguu kutoka Uhispania  na kupitia Ufaransa na kujikuta akifika Ubelgiji.