Friday , 15th Apr , 2022

Serikali ya Afrika Kusini imetangaza janga lililopiga mashariki mwa nchi hiyo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 300 kuwa ni kubwa ;

Janga hilo linahusisha mafuriko makubwa yaliyotokea mapema wiki hii, na kuua takribani watu 341 na kusababisha uharibifu mkubwa wa nyumba na biashara 

Uharibufu mkubwa umetokea katika eneo la Durban katika jimbo la KwaZulu-Natal , jiji ambalo ni la tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya watu nchini humo.

Rais Cyril Ramaphosa amesema kuwa janga hilo ni sehemu ya mabadiliko ya tabia nchi , lakini badhi ya wakazi wamelaumu miundombinu mibovu kusababisha mafuriko makubwa .

Kwa kujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini humo, mafuriko hayo yalitokana na kiwango kikubwa cha mvua kilichonyesha, ambapo kilikua ni  300mm iliyonyesha kwa saa 24 mfululizo tarehe 11 mwezi huu.   

Kiwango hicho ni kikubwa ikilinganishwa  na hapo awali , ambapo mafuriko yaliyotokea mwaka 2019 yalikua na kiwango kidogo cha mvua cha hadi  165mm.