Friday , 15th Apr , 2022

Baba Mzazi wa marehemu Maunda Zorro, Mzee Zahir Zorro anasema zamani kabla ya Maunda hajapata watoto alikuwa anasahau kama ni mwanamke kwa sababu alimfundisha mchezo wa Martial Arts baada ya kutoka jeshini. 

Mzee Zahir Zorro na marehemu Maunda Zorro kulia

Mzee Zorro amesema kitu kingine ambacho watu hawakifahamu kuhusu Maunda Zorro ni uwezo wake wa kuimba kwa nguvu na sauti yake nzito pia huimba akiwa na furaha tu asipokuwa na furaha hawezi kuimba.

Mazishi ya Maunda Zorro yatafanyika siku ya kesho Jumamosi Tuangoma Kigamboni.