Wednesday , 13th Apr , 2022

Takribani watu 53 wamepoteza maisha kufuatia maporomoko ya ardhi na mafuriko baada ya kimbunga Megi kupiga huko  nchini Philippines.

Vikosi vya uokoaji bado vinatafuta manusura wa wa janga hilo katika vijiji vilivyozungukwa na mafuriko toka siku ya jana, wakichimba kwenye matope na kuingia kwenye vilindi vya maji mengi.   
Ingawa kwa mujibu wa mamlaka  za nchi hiyo, idadi ya watu waliopoteza maisha inatarajiwa kuongezeka zaidi.  

Vijiji vilivyopo jirani na jiji la Baybay katikati mwa jimbo la Leyte vimeathiriwa vibaya na janga hilo. 
Mito iliyofurika maji mengi na hususani maji yanayotiririka kutoka mabondeni yamezika vijiji vingi katokea eneo hilo , huku wengi wakifukiwa wakiwa hai.  

Meya wa jiji la Baybay Jose Carlos Cari amesema kuwa eneo hilo la kijiji pekee, watu takribani 47 wamepoteza maisha.  

Katika kijiji kiitwacho Pilar, takribani asilimia  80 ya nyumba zimesombwa kuelekea baharini  .
Kitengo cha kitaifa cha maafa nchini humo kimeripoti vifo kusini mwa mikoa ya   Davao , Mindanao na katikati ya jimbo la Negros  

Mamlaka zinasema Zaidi ya watu 100,000 waliopo kusini na mashariki mwa visiwa vya Ufilipino wameathiriwa vibaya na janga hilo.  .
 Wengi wameyakimbia makazi yao kuanzia jumapili ya wiki jana wakati kimbunga kijulikanacho kama   Agaton kilipoanza.