
Kamanda wa kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro
Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro amebainisha kuwa mnamo Aprili 5, 2022 mtuhumiwa aliyetambulika kama Latifa Bakari mwenye umri wa miaka thelathini na tatu (33) mkazi wa Mabibo jijini Dar, aliachiwa mtoto na mdogo wake kwa lengo la kumlea mtoto huyo, na hapo ndipo mtuhumiwa alifanya mauaji hayo.
Aidha RPC Muliro ameongeza kwa kusema kuwa baada ya mtuhumiwa kubaini mtoto huyo amefariki kwa kumpiga, mtuhumiwa alichukua mwili wa marehemu, akaukunja na kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha akaudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side Ubungo,
Katika hatua nyingine Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata watu wanne (4) kwa tuhuma za kujaribu kuhujumu miundombinu ya Shirika la Umeme TANESCO ikiwemo Nyaya aina ya Copper kwa lengo la kuziuza.
RPC Muliro ameeleza kuwa watuhumiwa ambao ni Omary Ally (28) mkazi wa Tegeta na wenzake walikamatwa Aprili 10 mwaka huu na baada ya kuhojiwa na polisi walikiri kufanya vitendo hivyo vya kihalifu.