Monday , 11th Apr , 2022

Madiwani wa Manispaa ya Moshi wamepiga kura ya kumuondoa meya wa wa manispaa hiyo Juma Raibu kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili 

Kura 18 zimemuondoa madarakani Meya huyo kutokana na tuhuma nne zinazomkabili  ikiwemo tuhuma za rushwa katika  vibali vya ujenzi majengo katika halmashauri ya manispaa hiyo

Tuhuma nyingine zinazomkabili ni matumizi mabaya ya madaraka pamoja na mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu dhidi ya madiwani wenzake.

Mkurugenzi wa manispaa ya Moshi Rashid Gembe amesema kura 28 zilizopigwa na madiwani hao kura 18 zilikua za ndiyo na kura 10 zikisema hapana jambo ambalo lilihitimishwa kwa mujibu wa kanuni na Meya huyo kuong’olewa madarakani