Monday , 11th Apr , 2022

Bondia wa Tanzania Hassan mwakinyo amevuliwa ubingwa wa ABU uzito wa (Super-Welter Weight). Amevuliwa ubingwa huo baada ya kushindwa kuutetea ndani ya miezi 6 kama sheria na kanuni zinavyosema.

Mwakinyo alishinda ubingwa huo Mei 28, 2021 baada ya kushinda kwa Technical Knockout (TKO) dhidi ya Maiala Antonio raia wa Angola kwenye raundi ya 9. Lakini pia aliutetea Ubingwa huo kwa kumpiga Julius Indonga wa Namibia kwa TKO Septemba mwaka jana 2021.

Lakini pia ABU imemshusha Mwakinyo mpaka nafasi ya 3 kutoka ya kwanza kwenye viwango vya ubora barani Afrika akiwa wa 14 Dunia akiwa na nyota 4.