Wachimbaji katika mgodi wa Katarya mkoani Mara
Chama hicho kimesema hakitakuwa tayari kuruhusu wazara ya nishati na madini kuwatumia baadhi ya watu kwa ajili ya kuwaondoa wachimbaji wadogo wa madini katika mgodi wa Katarya huku kikipanga kufanya maandamano makubwa kama moja ya hatua ya kupinga unyanyasaji huo unaodaiwa kufanywa na serikali kupitia wizara hiyo ya nishati na madini.
Wakizungumza na wachimbaji hao wadogo katika kijiji cha Kataryo halmashauri ya Musoma wilayani Butiama viongozi wakuu wa chama hicho katika wilaya ya Butiama wamesema kuwa wizara hiyo ya nishati na madini imekuwa ikitumia serikali na vyombo vya dola wilayani humo kwa lengo la kutaka kuwanyang’anya wachimbaji maeneo hayo kinyume na maelekezo ya ilani ya CCM
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Nimrod mkono, akizungumza na maelefu ya wachimbaji hao amesema kitendo hicho kinachofanywa na wizara hiyo ya nishati na madini kutumia serikali na vyombo vya dola wilayani Butiama kuwaondoa wananchi hao kisha kugawa maeneo hayo kwa watu ambao amedai ni mawakala wizara hiyo kamwe hakitakubalika.
Tangu wananchi hao wagundue kuwapo kwa madini katika eneo hilo, serikali kupitia kwa mkuu wa wilaya ya Butiama ilifika na kuufunga mgodi huo hatua ambayo ilisababisha kamati ya siasa ya CCM wilaya ya Butiama kukutana na kutoa tamko la kuufungua mgodi huo ili kuwezesha vijana hao kuendelea na shughuli zao za uchimbaji wa madini.