
Ndg, Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa
"Nitatanguliza utumishi na siyo utukufu, hivi karibuni hivi, hivi siku za karibuni kuna desturi hivi, hivi vyeo tunavyovipata nchini vimekuwa vikiendana na utukufu hivi, na mbwembwe hivi. Ukifanya kazi vizuri utatukuzwa"- Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania.
Kinana ameyasema hayo leo Aprili 10, 2022 alipokuwa akiwahutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho katika hafla ya kumpokea mkoani Dar es salaam tangu alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Taifa.
Aidha, Katika hotuba yake ukumbini hapo. Ndugu Kinana amewasihi vijana nchini amabao ni wanachama wa Chama cha Mapinduzi kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama bila uoga. Kinana hakusita kuwahimiza viongozi wa chama hicho kuwapatia nafasi vijana wanaojitokeza na kusema kwamba wakati mwingine inakuwa ni vigumu kwao kupenya katika vinyangányiro.
"Niwasihi kundi la kwanza, vijana. Gombeeni nafasi za uongozi kwenye chama, na wakati mwingine wanapogombea wapeni nafasi kwasababu wakati mwingine kupenya inakuwa vigumu kwao"- Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti CCM Tanzania.