
Wananchi wa Kitongoji cha Msafiri kata ya Bungu wilayani Kibiti Pwani wakishiriki ujenzi wa kituo cha Polisi katika eneo hilo
Wananchi hao wanasema lengo ni kuimarisha hali ya ulinzi na usalama wilayani humo.
Akizungumza wakati wa zoezi la ujenzi wa kituo hicho kipya Mrakibu msaidizi wa Jeshi la Polisi na Mkuu wa kituo cha Polisi Bungu ASP Mohamed Mcheu amesema wameona kuna kila sababu za kujenga kituo hicho ili kuongeza nguvu ya utoaji huduma za kipolisi kwa askari wake katika kuhakikisha wanalinda wananchi na mali zao.
Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Ushirika wa zao la korosho mkoa wa Pwani Corecu Mussa Mng'eresa amesema awali wakati wa vuguvugu la mauaji ya Kibiti eneo la Bungu lilitumiwa na wahalifu kama kitovu cha mauaji katika wilaya ya Kibiti na Rufiji hivyo uamuzi wa kujenga kituo kikubwa eneo hilo unalenga kudhibiti aina ya matukio kama hayo yasijitokeze.