
Mkuu wa WHO Afrika Matshidiso Moeti, anasema idadi halisi ya maambukizi inaweza kuwa mara 97 zaidi ya kesi zilizothibitishwa.
Moeti anasema nchi nyingi za Afrika zimezoea magonjwa ya mlipuko, lakini idadi iliyoripotiwa haionyeshi ukweli wa ugonjwa huo.
Akitolea mfano nchi ya Afrika ya kusini anasema Takwimu za hivi karibuni zilizokusanywa na Baraza la Utafiti wa Matibabu la Afrika Kusini zinaonyesha kuwa idadi ya vifo inaweza kuwa mara tatu ya takwimu zilizoripotiwa.
Vipimo vya maabara vimebaini visa milioni 11.5 vya Covid na vifo 252,000 katika bara la Afrika, lakini kwa mujibu wa ripoti ya WHO wanasema huenda kufikia Septemba mwaka jana, watu milioni 800 walikuwa wameambukizwa.