Friday , 8th Apr , 2022

Los Angeles Clippers wanatarajia kucheza dhidi ya Minnesota Timberwolves siku ya April 12, kwenye mchezo wa hatua ya awali kupambania nafasi ya kuingia nane bora katika mbio za ubingwa wa NBA ukanda wa magharibi. 

Clippers wamefanikiwa kushika nafasi ya nane kwenye misimamo wa ligi ukanda wa magharibi baada ya kuifunga New Orleans Pelicans siku ya jumatatu huku washindani wao Timberwolves waliifunga Denver Nuggets leo kwa alama 127 dhidi  ya alama 121 huku nyota Anthony Edward akifunga alama 49 na kufanya rebound 6 na kutoa assist 8 kwenye mchezo huo.

Timberwolves wanamaliza nafasi ya saba ambapo mshindi wa mechi hiyo ataungana na atakayeshinda mtanange wa Pelicans dhidi ya San Antonio Spurs walioamliza nafasi ya tisa na kumi.

Kawhi Leonard anatazamiwa kurejea kwa upande wa Clippers walioifunga Timberwolves, mara tatu msimu huu na kupoteza mara moja, Paul George akianza mechi tatu na kukaa benchi kwenye mechi ambayo walipoteza.