Thursday , 7th Apr , 2022

Kiungo wa Yanga, Jesus Moloko ambaye alikuwa nje kwa muda kutokana na kuwa na majeraha amesema kuwa kwa sasa yupo fiti na anahitaji kuanza kikosi cha kwanza.

Kiungo wa Yanga, Jesus Moloko

Hayo yamesemwa na Kiungo huyo kuwa amefurahi kurejea na kuanza mazoezi na anamini kwamba kuwa fiti kurejea kwenye kikosi na kuendelea kutimiza majukumu yake ndani ya timu.

“Kikubwa ni kuona kila siku ninakuwa bora na nilipokuwa nje nilikuwa naona namna hali inavyokwenda na nilikuwa ninafanya mazoezi binafsi ili kuwa imara ,”.amesema Jesus Moloko.

Wakati alipokuwa nje kwa muda kiungo huyo mikoba yake ilikuwa mikononi mwa Said Ntibanzokiza,Farid Mussa na Chico Ushindi ambao walikuwa wakipewa majukumu na Kocha Mkuuu wa Yanga, Nasreddine Nabi