
Kocha wa Simba Pablo Franco Martin (kulia) akiongea na waandishi wa habari za michezo Jijini Tanga
Kocha Pablo amesema baada ya kumaliza mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya US Gendarmerie timu ilifanya mazoezi mepesi siku moja na leo kikosi hicho kikiwa jijini Tanga kitafanya mazoezi ya mwisho kabla ya mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union.
“Ratiba inatubana sana, juzi tumetoka kucheza mechi ngumu ya kimataifa jana tumefanya mazoezi mepesi asubuhi, mchana tukaanza safari ya huku. Tutapambana kuhakikisha tunapata ushindi’’ amesema kocha Pablo
Kwa upande wa hali ya kikosi kocha huyo raia wa Hispania amesema kuwa nohodha wa kikosi hicho John Bocco hatakuwa sehemu ya mchezo wa kesho baada ya kupata maumivu kwenye maandalizi ya mchezo uliopita dhidi ya US Gendermerie, mchezaji mwingine ni Hassan Dilunga nae ana majeruhi.