Wednesday , 6th Apr , 2022

Mabingwa mara nyingi wa NBA, Los Angeles Lakers watakosa hatua za Mtoano wa Ligi hiyo maarafu kama Play-off baada ya kukosa nafasi ya kushiriki hatua za awali ya michuano hiyo.

Ndoto za lakers zilizimwa na timu ya  Phoenix Suns na kuondoa matumaini ya

LeBron James kutwaa ubingwa wake wa tano msimu huu baada ya kuichapa Lakers kwa alama 121-110 katika dimba la Footprint Center.

Lakers ipo mbioni kuachana na kocha wake Frank Vogel msimu huu utakapo malizika  kutokana na mwenendo mbovu licha ya kuwa na staa aliyewahi kushinda tuzo ya MVP kama Russell Westbrook na wachezaji mahiri kama Anthony Davis.