
(Timu zilizofuzu kombe la dunia 2022 Qatar)
Timu zilizopo katika chungu cha kwanza ndio timu zitakazoongoza makundi hayo nane ya michuano hiyo na timu hizi zimepangwa kwenye namba za vyungu kufuatana na nafasi za timu husika katika viwango vya soka duniani vya FIFA vya mwaka huu.
(Chungu namba moja katika droo ya kombe la dunia)
Timu hizo zilizowekwa katika chungu namba moja ni wenyeji Qatar, Brazil wanaoongoza kwenye viwango vya soka dunaini kwasasa, Ubelgiji walio nafasi ya pili, Mabaingwa watetezi Ufaransa, Argentina, England, Ureno, na Hisapania hizi ndio timu zitakazoongoza makundi katika upangwaji huo.
Wachezaji wazamani magwiji wanaotarajiwa kuchezesha droo hiyo, pamoja na ni Cafu aliyewahi kua Nahodha wa Brazil, Lothar Matthaus wa Ujerumani, Jay-Jay Okocha wa Nigeria, Tim Cahill wa Australia, Abdel Ahmed Malallah wa Qatar, Ali Daei wa Iran, Bora Milutinovic wa Serbia na Rabah Madjer wa Algeria.
Michuano hiyo mikubwa zaidi ya mchezo wa soka duniani inatazamiwa kufanyika kuanzia Novemba 21 hadi Disemba 18 mwaka huu nchini Qatar.