
Wachezaji wa chelsea wakishangilia goli kwenye mchezo wa kombe la Carabao
Kipigo hicho cha mabao 2-0 kilikuwa ni cha pili kwa Conte tangu aanze kukinoa kikosi cha Tottenham katika michezo 12, na mara baada ya mchezo huo alikubali kuwa wapinzani wao walikuwa bora zaidi yao,
“Ulikuwa mchezo mgumu, mgumu tangu mwanzo, Chelsea walikuwa bora zaidi yetu. Ukilinganisha timu hizi mbili hakuna usawa, tunazungumzia timu iliyo tayari kushinda yani chelsea. leo tumeona tofauti kati ya timu hizo mbili.” amesema Antonio Conte
Kwa upande mwingine kocha huyo raia wa Italia ambaye aliwahi kukiknoa kikosi cha Chelsea katia ya mwaka 2016 hadi 2018 na hapo jana alirejea katika dimba la Stanford Bridge kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2018. Aliweka wazi kuwa anakibarua kikubwa cha kuboresha kikosi Tottenham.
“Kuna kazi kubwa ya kufanya kwa wakati huu, ni ngumu sana kuelewa ni sehemu gani inaihitaji kuboreshwa zaidi kwa sababu kuna maeneo mengi ya kuboresha. Tunahitaji muda mwingi na subira. Lazima tuwe wanyenyekevu, kuelewa hali ilivyo kwa sasa na kuendelea kufanya kazi ya kuboresha wachezaji wetu.”
Mabao ya Chelsea kwenye mchezo huo yamefungwa na Kai Haverts aliyefunga dakika ya 5 kabla ya beki wa Spurs Ben Davies kujifunga dakika ya 34 na kuipatia Chelsea bao la pili. Timu hizi zitakutana tena kwenye mchezo wa mkondo wa Pili utakao chezwa Januari 12, 2022 ambapo Tottenham watakuwa wenyeji wa mchezo huo.