Friday , 26th Dec , 2014

Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka amewataka watu wote waliyo jipatia ardhi kinyume na taratibu katika vijiji vya wilaya hiyo kurudisha haraka katika serikali za vijiji.

Mbunge wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka

Sendeka amesema kuwa ardhi inapaswa kurejeshwa haraka kwakuwa zoezi la kunyang’anya ardhi kwa watu waliyojilimbikizia ardhi waliyoipa kinyemela linaendelea na halitaangalia mtu wala wadhifa wake.

Ole Sendeka ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara uliyofanyika katika kijiji cha Narakawo na kuhudhuriwa na wakazi wa vjiji vya jirani amesema kuna baadhi ya watu wamefanya ardhi ya Simanjiro kama haina mwenyewe wanagawana kwa kupitia viongozi wasiyo wadilifu na kuwaacha wananchi wakiteseka na kwamba tabia hiyo haitavumilika.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Narakawo Tumaini Ndinga amesema yeye kama mwenyekiti atahakikisha kuwa anasimamia haki kwa watu wote na hatamfumbia macho mtu anayeenda kinyume kwani kiongozi mzuri ni anayejali jamii kuliko maslahi binafsi na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Simanjiro Brown Ole Suya amewata viongozi wa CCM kufanyakazi kwa umakini kwani wakati huu wa vyama vingi hakuna siasa ya mchezo.