Monday , 22nd Dec , 2014

Staa wa muziki Joh Makini, baada ya kupokea maoni tofauti kuhusiana na video yake ya ngoma ya 'I See Me', amesema kuwa hiyo inatokana na picha ya tofauti ambayo mashabiki walikuwa nayo kuhusiana na ngoma yenyewe.

Msanii wa Bongofleva nchini Tanzania Joh Makini

Joh Makini amesema kuwa, ni ngumu sana wakati mwingine kuiweka video katika mfumo ambao utaridhisha kila mtu, huku akikazia kuwa ni video ambayo imegharamiwa kama nyingine zote zile.

Kwa sasa rapa huyu amerejea kwa kishindo na video ya ngoma inayokwenda kwa jina XO ft G Nako, kazi ambayo tayari imeanza kueleweka mitaani.