Saturday , 13th Dec , 2014

Timbulo, Staa wa Bongo Flava anayefanya poa katika chati mbalimbali za muziki na ngoma yake ya Nakumiss Miss, amesema kuwa kwa sasa ameamua kuwa mbali na mambo ya mahaba niuwe na malavi davi, kitu ambacho kimemsaidia kumuweka mbali na skendo.

Timbulo kazini

Staa huyu amesema kuwa, amegundua kuwa kwa sasa anahitaji kujiweka karibu zaidi na muziki, huku akikiri kuwa tabia yake ya uwazi sana, vilevile umri ndio vilivyochangia yeye kuhusishwa sana na totoz, hususan kutoka katika tasnia ya Bongo Movie.

Kwa upande mwingine pia, Timbulo akaichana eNewz kuwa, nakumiss Miss ndio project yake ya pili na ya kumaliza mwaka huu, tayari kabisa kwa mashambulizi mapya mwezi Januari.

Tags: