Picha ya Mchezaji Jonas Mkude
Kiungo mkabaji huyo ameonekana na wachezaji ambao tayari wamewasili kambini tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano.

Kocha wa timu hiyo Didier Gomes aliagiza wachezaji wote kuingia kambi wiki hii ili kuanza maandalizi ya msimu ujao ambao inaelezwa kuwa kambi yao itawekwa nchini Morocco.



