Friday , 6th Aug , 2021

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amelazwa hospitali iliyopo nje ya gereza kwa ajili ya uangalizi wa matibabu, mamlaka za magereza zimeeleza.

Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma

Taarifa ya tasisi yake imesema kwamba hali hiyo ni utaratibu wa kawaida wa kuangalia afya yake mara kwa mara, hivyo hakuna haja ya kuibua hofu.

Mamlaka za nchi hiyo zimesema kiongozi huyo wa zamani wa taifa Zuma anatibiwa kwenye hospitali ya kijeshi.

Rais huyo wa zamani kwa sasa anatumikia kifungo cha miezi 15 jela tangu Julai 7 mwaka huu, kwa kukaidi amri ya Mahakama.