Monday , 12th Jul , 2021

Asubuhi ya leo Julai 12, 2021 tumeamka na story ya msanii Linah Sanga 'Official Linah' baada ya kumtolea povu na siri nzito ya CEO wa lebo ya Konde Gang Harmonize kwa kumtaka kuwa naye kwenye mahusiano.

Picha ya msanii Linah na Harmonize

Linah amemchana Harmonize kupitia page yake ya Instagram kwa kuandika ujumbe ufuatao kisha kuufuta baada ya muda mfupi.

"Harmo Harmo nakuita tena, au kwa sababu sikutaki umekuwa ukinitafuta kwa njia zote nimekukataa na unakuja kwa njia huyo ya Seven kama kifua kumbe huna lolote

"Umeharibu familia ya wenzako leo ukaona haitoshi unakuja na kwangu, sijui hata kama ulizaliwa wewe au ulitapikwa, mwanaume una roho kama ya wanyama sikupendi nakuchukia" ameongeza