Jumanne , 17th Dec , 2024

Nyota wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Atalanta ya nchini Italia inayoshiriki ligi kuu nchini humo Serie A ametangazwa kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2024 katika sherehe zilizofanyika Marrakech, Morocco jana.

Lookman amewashinda Achraf Hakimi wa PSG na timu ya taifa ya Morocco,Serhou Guirassy wa Borrusia Dortmund na timu ya taifa ya Guinea na Ronwen Williams wa Afrika ya Kusini.

Mshambuliaji huyo wa Atalanta na Nigeria amefanikiwa kushinda tuzo hizo baada ya kufanya vizuri akiwa na timu ya taifa ya Nigeria katika michuano ya AFCON ya 2023 aliiwezesha The Super Eagles kufika fainali ambayo ilipoteza mbele ya Ivory Coast pamoja kuiwezesha Atalanta kushinda taji la Europa akifunga magoli mawili katika mchezo wa fainali dhidi ya Bayern Leverkusen.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Chalton Athletic,Everton,RB Leipzig,Fulham na Leicester City ameshinda tuzo hiyo akimpokea raia mwenzake wa Nigeria Victor Osimhen aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2023.

Babra Banda wa timu ya taifa ya Wanawake Zambia ameshinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika kwa upande wa Wanawake.

Ronwen Wiliiams akishinda tuzo ya Mchezaji bora wa mwaka wa Africa kwa Wchezaji wanaocheza ndani Afrika pamoja na tuzo ya Golikipa bora wa mwaka kwa upande wa Wanaume.

Lookman anakuwa raia wa sita kutoka Nigeria kushinda tuzo hiyo ya Mchezaji bora wa mwaka wa Afrika.Inakuwa mara ya pili kwa Wachezaji wa Nigeria kushinda tuzo ya Mchezaji bora wa Afrika kwa mara mbili mfululizo mara ya kwanza ilitokea kwa Nwanko Kanu 1997 na  Victor Ikpeba 1997.Victor Osimhen alishinda tuzo hiyo mwaka 2023 na Ademola Lookman ameshinda tuzo hiyo 2024.