Friday , 5th Dec , 2014

Ulimwengu wa mitindo kwa upande wa Hapa Tanzania unatarajiwa kupambwa na tukio la kihistoria leo hii ambapo maonesho makubwa ya mitindo ya Swahili Fashion Week yameanza rasmi na kuendelea kwa siku tatu mfufulizo katika Hoteli ya Sea Cliff DSM.

Maonesho ya mavazi na mitindo Swahili Fashion week Tanzania

Katika jukwaa leo wabunifu Afrikadndrl, Ailinda Sawe, H&, Mabinti Centre, EDC, Handmade TZ and Can Wear na Sabina Mutsvasi ndio watahusika katika kuonesha mitindo yao.

Mbali na Maonyesho ya mitindo kutoka kwa wabunifu mbalimbali, Swahili Fashion Week pia itahusisha tuzo kwa wanaofanya vizuri katika vipengele mbalimbali vya mitindo na vilevile tamasha la manunuzi ya kazi mbalimbali za mitindo, tukio litakalochukua nafasi siku ya Jumapili.