Sunday , 30th May , 2021

Mbunge wa Sumbawanga Aeshi Hilaly ameitaka Serikali kuwalipa fidia wavuvi wa dagaa katika ziwa Tanganyika na Nyasa ambao walichomewa nyavu zao.

Mbunge wa Sumbawanga Aeshi Hilaly

Aeshi ameeleza hayo kwenye mahojiano na East Africa TV ambapo amesema serikali imeumiza sana watu wengi huko nyuma hivyo inabidi iwalipe fidia.

''Watu walichomewa vyavu wakati vipimo vikiwa sawa ila serikali ndio ilitofautiana kwa vipimo vya TBS na Wizara, lakini hata watu walipolalamika kwamba wananunua madukani na risti wanazo lakini serikali haikwenda kuchukua hatua kwa wauzaji na mwisho wa siku watu wamefilisika,'' amesema Aeshi. 

Zaidi tazama video hapo chini