Mkuu wa Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Nishati na Madini Bi. Badra Masoud kushoto akisisitiza Jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkuu wa Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Nishati na Madini Badra Masoud, wakati anazungumza na Wanachama wa Vilabu vya Habari kutoka Mikoa ya Lindi na Mtwara, waliokutana Kilwa Masoko ambako ameelezea mafanikio ya sekta hiyo pamoja na mipango ya Serikali ya kusambaza umeme vijijini chini ya mpango wa Usambaaji wa umeme vijijini ujulikanao kama REA.
Amesema,kufikia asilimia 36 hivi leo ni mafanikio kwa kuwa lengo la Serikali lilikuwa ifikapo mwaka 2015 upatikanaji wa umeme ufikie asilimia 30,na kuongeza kuwa hata uzalishaji wake umeongezeka,ndio maana hivi sasa jitihada kubwa ni kufikisha umeme kwa watumiaji wa vijijini.
Kwa mujibu wa Msemaji huyo wa Wizara ya Nishati na Madini,katika kuharakisha usambazaji wa umeme kwenye Mikoa ya Lindi na Mtwara,wateja wamepata punguzo la kuunganishiwa kwa bei ya Sh.99,000/- badala ya Sh.Laki moja kama ilivyo sehemu zingine hapa nchini